HOTUBA YA GAVANA WA GATUZI LA MERU MHESHIMIWA PETER MUNYA KUHUSU HALI YA GATUZI LA MERU MWAKA WA 2017

HOTUBA YA GAVANA WA GATUZI LA MERU MHESHIMIWA PETER MUNYA KUHUSU HALI YA GATUZI LA MERU MWAKA WA 2017    

COUNTY GOVERNMENT OF MERU OFFICE OF THE GOVERNOR When replying please quote Meru County Headquarters Email:merucounty@meru.go.ke P.O Box 120-60200 Meru County

HOTUBA YA GAVANA WA GATUZI LA MERU MHESHIMIWA PETER MUNYA KUHUSU HALI YA GATUZI LA MERU MWAKA WA 2017. Waheshimiwa wabunge wa gatuzi la Meru, Wananchi wenzangu, Mabibi na mabwana Siku ya leo nina furaha kujiunga nanyi katika hafla hii ya kutathmini maendeleo na uafikiaji wa malengo yetu kama gatuzi la Meru. Ni takribani miaka mine sasa tangu mfumo wa serikali za kaunti kuanzishwa humu nchini. Kama Gavana wa kwanza nimechukua hatua za kuhakikisha msingi bora wa utandawazi wa ukuaji hali kadhalika ufanisi wa kaunti yetu. Hivyo basi tunatazama na kuichunguza kwa kina safari hii tuliyoianza kuhakikisha wananchi na wakaaji wa Meru wamenufaika kikamilifu kutokana na huduma za serikali yangu. Mbali na changamoto mbalimbali zilizotukabili, serikali yangu inatazama kwa furaha hatua mahususi za kimaendeleo tulizopiga kuboresha maisha ya jamii yetu kwa kustawisha miundomsingi ya utendakazi bora na kuafikia kwa malengo ya serikali na sera tulizoahidi wananchi. AFYA Katiba ya Kenya iliyopitishwa mwaka wa elfu mbili na kumi (2010) inaamrisha serikali ya kitaifa pamoja na zile za kaunti kustawisha huduma za afya kufikia wakenya wote kwa sababu ni haki yao ya msingi. Kila mwaka, serikali yangu imeekeza asilimia arobaini (40%) ya mgao wa fedha tunazopokea katika gatuzi letu kustawisha nguzo sita muhimu za ukuaji wa sekta ya afya. Uongozi na usimamizi. Sekta ya afya ya Meru inaongozwa na mfumo wa kisheria uliopitishwa na bunge la Kaunti ambayo nilitia sahihi ukawa sheria. Sheria hii inaangazia kutatua changamoto za kipekee za jamii yetu. Kwa miaka mine sasa serikali yangu imeimarisha usimamizi wa sekta ya afya katika vituo vyote vya afya kwa kuteua bondi za usimamizi katika hospitali kumi na sita (16), kamati za vituo vya afya (health centers) thelathini na mbili (32), na zahanati (dispensaries) mia moja thelathini na tano (135). Bondi na kamati hizi husaidia katika mipango, na utekelezaji wa miradi, kadhalika ukusanyaji wa maoni kuhusu huduma. Utoaji huduma. Katika kipindi cha miaka mine serikali yangu imejenga na kuboresha vituo mbalimbali vya afya. Kama matokeo ya juhudi za serikali yangu, wakaaji wa Meru usafiri kilomita saba kupata huduma za afya ikilinganishwa na kilomita kumi na tatu kabla ya mfumo wa ugatuzi kuanzishwa.Kwa sasa tuko na hospitali kumi na sita(16), vituo vya afya(health centers) thelathini na tatu (33), na zahanati(dispensaries) mia moja thelathini na sita. Miaka mine iliyopita kulikuwa na zahanati themanini na tisa(89), na tumejenga arobaini na saba (47) zaidi ambazo ni kama ifuatavyo; • Ntirimiti, Maritati,Kithithina, Sirimon,Njuruta, Kimbo, Ntumburi, Mutunyi na Nkando katika Gatuzi ndogo la Buuri. • Luciuti, Leeta, Nairuru, KK Etama, Muromutua na Kileera katika Gatuzi ndogo la Igembe Kaskazini. • Giika katika Gatuzi ndogo la Igembe kusini. • Thinyaine, Machegene na Kaliati katika Gatuzi ndogo la Tigania Magaribi. • KK Mwethe, Akaiga, Kaathi, Mbaranga, Kandebene na Matabithi katika gatuzi ndogo la Tigania Mashariki. • Gatakene, Baranga, Ithitwe, Kigane, Kairiene, Mwichiune, Mworoga, Muungu na Kiamweri katika Gatuzi ndogo la Imenti Kusini. • Gankere, Ndiine, Runogone, Chabuene, Nthuungu na Kianjuri katika Gatuzi ndogo la Imenti Kaskazini. • Gitauga, Mwanika na Marathi katika Gatuzi ndogo la Imenti ya Kati. Kabla ya Agosti 2017, tunamalizia na kufungua zahanati ishirini na tisa zaidi . Baadhi yazo ni Ndoleli, Kamweline, Kamboo, Munanda, Kachuuru, Murweti, Kianda, Kaani ka Rui, Makandi, Karii, Muchuune, Mucege, Igandene, Kiarene, Kambiti, Mutunguru, Mulathankari, Mwiteria, Ruiga, Chaaria, Runywene, Kinjo, Mbui Njeru, Kiambogo, mbaranga, Luuma, Muula, Menoe na Ntemwene. Tumeongeza idadi ya vitanda vya kulaza wagonjwa kutoka mia saba na ishirini (720) mwaka wa elfu mbili na kumi na tatu (2013) hadi elfu moja na themanini na nane (1088) mwaka huu. Tulinunua vitanda spesheli mia mbili themanini (280) vya hospitali kuu ya kimafunzo ya Meru pamoja na zile za gatuzi ndogo zikiwemo Githongo, Nyambene, Kanyakine na zinginezo. Ili kuhakikisha matumizi bora ya rasilmali, na uendeleaji wa huduma, serikali yangu itazindua mradi wa wodi ya gorofa saba (7 storey integrated ward) katika hospitali kuu ya mafunzo ya Meru.Mradi huu ambao tutauzidua kwa muda wa wiki moja, utaongezea idadi ya vitanda kutoka mia nne na sitini(460) kwa sasa hadi elfu moja mia tano(1500) baada ya kukamilika. Jumla ya idadi ya vitanda vya kulaza wagonjwa inatarajiwa kufika elfu mbili (2000) kufikia mwaka wa 2019. Hii leo Kaunti ya Meru ni ya pili nchini kwa viwango vya chini vya maafa ya watoto wanaozaliwa kwa kiwango cha mia mbili na mbili(202) kwa kila watoto laki moja (100,000) wanaozaliwa. Kiwango cha kitaifa ni mia tatu sitini na mbili (362) kwa kila laki moja ya wanaozaliwa. Tunaazimia kupunguza kiwango hiki zaidi hadi mia moja arobaini na mbili (142) kufikia mwisho wa mwaka huu wa 2017. Vifaa vya kuhifadhi watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao (incubators) vimenunuliwa na kuwekwa katika kila hospitali ya gatuzi ndogo ili kuimarisha matokeo ya huifadhi wa watoto wadogo. Ili kuhakikisha kuwa wamama wamejifungua kwa njia salama na katika mahali safi, tumefungua vyumba kumi na viwili (12) vya kujifungulia kwa kipindi cha miaka mine iliyopita na kufikisha idadi yake kuwa arobaini na nane (48). Vyumba hivi vimefunguliwa; Kiburine, Nthambiro, Amugaa, Lailuba, Kiarago, Kaongo, Ontulili, Mulika, Njuthine, Kionyo na Kiguchwa. Kama njia ya kuboresha uwezo wa vipimo na ukaguzi wa magonjwa, serikali yangu imenunua na kuweka mashine spesheli za vipimo, na uchukuaji wa picha katika hospitali kuu ya Meru na za gatuzi ndogo. Tumenunua na kuweka mtambo wa kiatomatiki wa baokemia wa mahabara za Githongo, Timau, Muthara, Nyambene, Mutuati, Kanyakine na Miathene. Vifaa vya kisasa vya uchukuaji picha (X-Ray Machines) vimenunuliwa na kuwekwa katika hospitali ya kimafunzo ya Meru pamoja na zile za gatuzi ndogo. Hospitali ya Meru kwa sasa ina mashine zinazofanya kazi kama vile CT Scan na mashine za x-ray za kidigitali. Kukamilisha haya na ufuatiliaji wa wamama wajawazito, serikali yangu imenunua mitambo ya kupeleleza mimba (Ultra Sound) na inafanya kazi hospitali za Mutuati, Muthara, Miathene, Githongo, na Kanyakine katika gatuzi ndogo husika. Wakaaji wa gatuzi letu wenye matatizo ya figo hawalazimiki tena kusafiri Nairobi na kusubiri wiki kadhaa kutafuta huduma katika hospitali kuu ya Kenyatta. Huduma za uoshaji figo (Renal dialysis services) zinapatikana katika hospitali kuu ya kimafunzo ya Meru na gharama hiyo kulipwa na NHIF ya jumla. Kabla ya mwisho wa mwezi huu, huduma hii pia itaanzishwa katika hospitali ya Nyambene kama njia ya kupunguza msongamano. Kadhalika, serikali yangu imenunua magari kumi na tatu (13) ya kubebea wagonjwa na kuwekwa mahali mwafaka ili kushughulikia maswala ya dharura. Kwa sasa tuko na magari ishirini na saba (27) ya kusafirisha wagonjwa na manne (4) zaidi yananunuliwa. Huduma za kusafirisha wagonjwa hutolewa bure kwa wale walioelekezwa kutafuta huduma za dharura na wafanyakazi wetu wa afya. Wale walioelekezwa na vituo vya kibinafsi hulipa ada ndogo ambayo hutuwezesha kuhifadhi ubora wa magari na vifaa vilivyomo. Magari haya yamewekwa Hospitali kuu ya mafunzo ya Meru, za Mutuati, Kangeta, Timau, Miathene, Kanyakine, Kinoro hospitali za gatuzi ndogo, na vituo vya afya vya Mweronkanga na Nthambiro. Tuko katika harakati za kukabidhi magari tuliyonunua ya kusafirisha wagonjwa hospitali ya Kibirichia pamoja na vituo vya afya vya Amugaa, Karama na Kaongo hivi karibuni. Wakati tulianza mfumo wa ugatuzi, tuliridhi vyumba vya kuhifadhia maiti ambako mili ilikuwa inaoza kwa sababu ya vifaa duni. Serikali yangu ilinunua vifaa vya hali ya juu na vya kisasa. Katika hospitali kuu ya kimafunzo ya Meru, kuna uwezo wa kuhifadhi mili sabini na tano (75), hospitali ya Nyambene, mili thelathini (30) na hospitali ya Miathene mili kumi na tano (15). Hospitali ya Kanyakine itapata chumba chenye uwezo wa kuhifathi mili thelathini (30) na itakuwa tayari ifikapo Agosti mwaka huu. Mwaka ujao wa kifedha tutajenga vyumba vya kuhifadhi maiti vya Timau, Mutuati, Githongo, Muthara na Mikinduri ili kupunguza safari ya wananchi kusafirisha mili ya wapendwa wao kwenda kuzika. Umeme ni muhimu kwa vifaa na mitambo ya huduma kwa hospitali zetu. Ili kuzuia kupoteza maisha kwa wale wagonjwa walio katika mitambo maalum inayotumia umeme, serikali yangu imenunua mitambo ya kuzalisha umeme ya jenereta kwa hospitali za Meru, Nyambene, Mutuati, Kangeta, Muthara, Mbeu, Naari, Timau, Giaki, Mikinduri na Kinooro, na vituo vya afya vifuatavyo;Kiburine, Gatimbi, Karama, Laare na Akachiu. Wafanyakazi wa idara ya afya. Gatuzi letu linaongoza kwa idadi ya mahospitali humu nchini. Hii inamaanisha idadi kubwa ya wafanyakazi wa afya inahitajika ili kutoa huduma bora kwa wananchi.Kwa sasa tuna wafanyakazi zaidi ya elfu mbili (2,000) wakiwemo; • Madaktari mia moja arobaini na watano(145). • Wauguzi elfu moja mia moja na thelathini(1130). • Maafisa wa kiafya(clinical officers) mia mbili na watano(205). • Maafisa wa mahabara(lab technologists) mia moja sitini na moja(161). • Maafisa wa afya ya umma (public health officers) mia moja arobaini na watatu (143). Meru ilikuwa kaunti ya kwanza kuwaajiri kwa misingi ya kudumu wauguzi mia mbili arobaini na watatu (243) walioajiriwa na serikali kuu kwa mpango maalum wa ukuaji wa uchumi (Economic Stimulus Program) kama wafanyakazi wa kadarasi. Baada ya kushika hatamu za uongozi, serikali yangu iliajiri madaktari hamsini na wawili (52) zaidi na wauguzi mia nne na saba (407). Kwa sasa bajeti ya mishahara ya wafanya kazi wa afya ni bilioni moja nukta sita (1.6b kshs) na itazidi bilioni mbili nukta moja sita (2.16b) baada ya nyongeza za mishahara zilizoafikianwa kutekelezwa. Dawa. Serikali yangu imejizatiti kuhakikisha kuwa madawa ya kutosha yanapatikana katika vituo vyetu vya afya.Kwa mfano katika bajeti ya mwaka huu, tumetumia milioni mia mbili na ishirini (220,000,000) kwa ununuzi wa madawa ikilinganishwa na milioni hamsini na saba (57,000,000) mwaka wa 2012-2013 wa matumishi ya fedha za kiserikali.Hilo ni ongezeko la asilimia mia tatu themanini na tano nukta tisa (385.9%) kwa fedha tunazoekeza kwa ununuzi wa madawa kwa miaka mine iliyopita. Kufadhili huduma za afya. Huduma za afya katika gatuzi letu hupokea mgao wa takriban billion mbili kila mwaka. Kulingana na sera ya kitaifa ya afya, tunatekeleza ugawaji wa gharama (cost sharing) ili kuleta huduma za bei iliyopunguzwa bila kunyima huduma kwa mwananchi yeyote asiyekuwa na uwezo wa kulipa. Waheshimiwa wabunge, kupitia usimamizi bora na uwajibikaji, tumeboresha ukusanyaji ada kutoka milioni kumi na nne (14) mwaka wa 2013 hadi milioni thelathini na mbili (32) kila mwaka kwa sasa. Siku ya leo ninatangaza kuwa vituo vyote vya zahanati(dispensaries) vitatoa huduma zao bure , na hakuna malipo yanapaswa kutozwa nananchi hata ya mahabara. Ninaamrisha maafisa husika katika idara ya Afya kutekeleza amri hii mara moja. Kadhalika tunatumia mbinu ya kuhusisha jamii katika miradi ya kiafya, jambo ambalo limesababisha gharama ya ujensi kupungua kwa asilimia sitini (60%). Kupitia ofisi ya Mama wa kwanza wa gatuzi letu, tumeweza kuchunguza na kufanyia watu zaidi ya sabini na moja elfu, mia nne sabini na tisa (71,479) vipimo vya saratani, na jumla ya watu elfu moja na mia mbili hamsini na wanane (1258) wakapatikana na chembechembe za saratani. Mia nne wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali kuu ya Meru. Wengine elfu moja mia tatu walitibiwa na wakaruhusiwa kwenda nyumbani.Hata sasa tunawaomba mtembelee hospitali hiyo kwa uchunguzi, matibabu na mawaidha kuhusiana na janga hili la saratani. Vilevile huduma mbalimbali za kutibu saratani hupatikana katika hospitali ya Meru kama vile; Onkolojia ya kiupasuaji(surgical oncology), na kemotherapia(chemotherapy). Ni muhimu kutambua kwamba bali na hospitali kuu ya Kenyatta jijini Nairobi na hospitali chache za kibinafsi, ni hospitali kuu ya kimafunzo ya Meru pekee ambayo hutoa huduma hizi. Ili kupambana na janga hili zaidi, tumeanzisha sajili ya saratani (Cancer Registry) hapa Meru. Hii imetusaidia kufanya utafiti tukishirikiana na shirika la utafiti wa kiafya la Kenya Medical Research Institute (KEMRI) Watu walio na changamoto ya upungufu wa aina mbalimbali katika mili yao wamepata vifaa visaidizi elfu mbili mia tatu ishirini ma moja (2321) kutoka kwa ofisi ya mama wa kwanza wa gatuzi letu, kama vile vitiguru (wheel chairs), viungo bandia vya miguu na mikono kwa wengine miongoni mwa misaada mingine kutokana na juhudi za Mama wa kwanza wa gatuzi letu. Pia kampeini dhidi ya trakoma na maradhi ya macho imeendeshwa na kati ya watu elfu kumi mia moja na kumi na watano (10,115) waliofanyiwa uchunguzi, elfu mbili mia nne hamsini na mmoja (2,451) kati yao walipatikana na maradhi ya trakoma. Baadhi yao elfu mbili na kumi na sita wamefanyiwa upasuaji kurekebisha hali hiyo. Kwa sababu ya juhudi mbalimbali za serikali yangu, viwango vya malaria vimepungua hadi asilimia moja (1%) ya waliotibiwa mwaka wa 2016 ikilinganishwa na asilimia thelathini na tatu (33%) mwaka wa 2013. Idadi ya vyoo kwa kila familia imeinuka kutoka asilimia sitini na mbili(63%) mwaka wa 2013 hadi asilimia tisini na nane (98%) mwaka wa 2016. Vilevile maradhi ya kuhara (diarrhea) yamepungua kutoka asilimia kumi na nne (14%) mwaka wa 2013 hadi asilimia tano (5%) mwaka wa 2016. MAJI Kwa idara ya maji, serikali yangu inaendelea kuinua viwango vya maji safi yanayofikia mwananchi kwa lengo la kuweka mfereji kwa kila mboma kufikia mwaka wa elfu mbili na ishirini na moja (2021) kuambatana na malengo ya maendeleo endelezi. Serikali imestawisha miradi mipya ya maji hali kadhalika kuboresha miradi iliyokuwemo katika jamii ili kuimarisha usambazaji wa maji kwa wakaaji. Katika Gatuzi ndogo la Igembe kusini, mradi wa maji wa Kibilaku eneo la Kiegoi umejengewa sehemu ya mapokezi (intake) na mifereji kuongezwa zaidi ili kuhudumia sehemu za soko la Kiegoi na Kibilaku. Vilevile tangi lenye uwezo wa kuhifadhi lita laki mbili, elfu ishirini na tano (225,000 liters) limejengwa katika soko la Kiegoi ili kufikisha maji katika taasisi zilizoko eneo hilo. Huko Athiru gaiti, mradi wa maji wa Gatungu umestawishwa. Tangi lenye uwezo wa kuhifadhi lita laki mbili, ishirini na tano elfu (225,000 liters) limejengwa katika Kirimampio wadi ya Akachiu Katika Igembe ya kati, ksima cha maji kimechimbuliwa eneo la Kalimbene wadi ya Kangeta na tangi lenye uwezo wa kuhifadhi lita laki mbili, ishirini na tano elfu (225,000 liters) limejengwa na sehemu ya usambazaji kuundwa. Mradi wa maji wa Njia water supply awamu ya kwanza umefanyika katika wadi ya Njia. Hii ni pamoja na ujensi wa tangi lenye uwezo wa kuhifadhi lita laki mbili, ishirini na tano elfu (225,000 liters) na tangi linguine shule ya msingi ya Nchunguru la kusambaza maji Maili tatu na maeneo ya Antubeiga. Tangi lenye uwezo wa kuhifadhi lita laki mbili, ishirini na tano elfu (225,000 liters) limejengwa huko Kabuitu wadi ya Igembe Mashariki. Igembe Mashariki, kisima kimechimbuliwa katika shule ya msingi ya Matiandui na mifereji kutolewa itakayosambaza maji hadi Kanyakine na Kabuitu na hivyo basi kuwafaa watu elfu moja (1,000). Kisima cha Githongo wadi ya Athiru rujine kilichimbuliwa na kustawishwa na usambaza maji sehemu za wadi ya Athiru Rujine na zile za Igembe mashariki. Awamu ya pili ya Njia inaendelea kushughulikiwa na itahusu kuchimbua visima viwili eneo la Thuuru, kuchimbua kisima eneo la Nchunguru, kuboresha kisima cha Shule ya msingi ya Nchunguru, ujensi wa tangi lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita hamsini elfu (50,000 liters) eneo la Thuuru, na kutia mifereji kuhudumia maeneo ya Kithare, Muringene, Maili-tatu, Antubeiga, na Itwamwari. Mradi huu utafaidi takriban watu elfu kumi (10,000). Mradi wa Kithing’ang’u wadi ya Akirang’ondu pia umeboreshwa kwa ujensi wa stesheni ya kutoa maji (pumping station) katika chemichemi ya Kithing’ang’u. Isitoshe ujensi wa tangi lenye uwezo wa kuhifadhi lita elfu mia moja (100,000) unaendelea na mifereji imetolewa kusambaza maji haya hadi soko la Kathelwa. Mradi huu utafaidi watu elfu tatu (3,000). Kisima kimechimbuliwa katika soko la Kangeta na mifereji ya usambazaji kuwekwa kutoka soko la Kangeta hadi eneo la Keiya mradi utakaowanufaisha watu elfu tatu. Serikali vilevile imekamilisha mradi wa maji wa Gatwe ulio+anzishwa na idara ya sehemu kame na kuachwa bila kukamilika. Mradi huu unahudumia watu wa Malaene wadi ya Antubetwe Kiongo. Gatuzi ndogo la tigania mashariki, tangi lenye uwezo wa kuhifadhi lita laki mbili, ishirini na tano elfu (225,000 liters) limejengwa Karachi wadi ya Muthara. Pia kuboreshwa kwa mifereji ya Muthara-Muriri inayoleta maji kutoka mto Thangatha hadi soko za Muthara na Muriri. Zaidi ya hayo, kisima kimechimbuliwa eneo la Rumanthi. Ili kusambaza maji maeneo ya Luuma na Lanyiru, maji yatahifadhiwa katika tangi la lita laki mbili, ishirini na tano elfu (225,000 liters) katika mlima wa Luuma. Mradi huu utawafaa watu elfu tatu (3,000). Zaidi ya hayo, kazi ya mradi wa chemichemi za Mikorwe, ujensi wa tangi la lita laki mbili, ishirini na tano elfu (225,000 liters) huko Muti utikirira na urekebishaji wa mifereji ya urefu wa kilomita mbili kufikisha maji soko za Muthara na muriri na vitongoji vyake, pamoja na uboreshaji wa mapokezi ya Maburwa na mifereji ya kusafirisha maji hadi shule ya msingi ya Kaongo. Tangi lenye uwezo wa kuhifadhi lita laki mbili na ishirini na tano elfu (225,000 liters) limejengwa katika wadi ya Karama. Ujensi wa sehemu ya kupokelea (intake) katika mto Liutu umekamilika. Mradi huu utafaidi watu elfu mbili (2,000) Kutoka Liutu, Kiinjo, Mbaranga hadi shule ya msingi ya Laibocha. Uboreshaji wa chemichemi za Michii mikuru unaendelea kwa sasa. Uwekaji wa mifereji kuelekea kibore na tangi la Lukununu pia unaendelea na utawafaa zaidi ya watu elfu tano (5,000) eneo hilo. Ujensi wa mapokezi (intake) ya Muramba ya unyunyiziaji wadi ya Thangatha unaendeleana utaunganishwa na mifereji ya urefu wa kilomita kumi na moja (11). Gatuzi ndogo la Tigania Magharibi, urekebishaji wa utandawazi wa mifereji ya maji Kianjai kutoka mto Thangatha hadi Kianjai umefanyika. Tangi lenye uwezo wa kuhifadhi lita laki mbili na ishirini na tano elfu (225,000 liters) limejengwa eneo la mlima Muthunanga karibu na soko la Miathene kuhudumia watu wa Kariokor. IDARA YA MAJI, MAZINGIRA NA RASILI MALI. Tangi lingine limejengwa Ngundune ili kuhudumia soko la Ngundune hadi zahanati ya Thinyaine. Vilevile visima viwili vimechimbuliwa katika shule ya msingi ya Lubunu katika wodi ya Nkomo. Maji ya visima hivi, yatasukumwa kwa tangi la uhifadhi lililo katika mlima Kieru na kisha mifereji ya usambazaji kuwekwa ili kuhudumia soko la Nchiru na eneo la Mituntu. Mradi huu utafaidi Zaidi ya wenyeji elfu kumi. (10,000). Katika wodi ya Akithi, kisima kimechimbuliwa katika Barubaru - Mwerongundu ili kuhudumia eneo hilo. Vilevile mtambo wa kawi ya jua umewekwa wa kusukuma maji, umewekwa katika mradi wa Kathima Katika gatuzi ndogo la Buuri, tumeongeza laini saba za miferji huko Sirmon, ambazo zina tarajiwa kufaidi Zaidi ya jamii mia moja (100) katika wodi ya Kisima. Katika soko la Ngusishi, tumejenga tangi la lita elfu mia mbili ishirini na tano (225000), na stesheni ya usukumaji maji pamoja na usambazaji kukamilika. Zaidi ya hayo, matangi mebgine ya lita elfu mia mbili na ishirini na tano ( 225000) yamejengwa huko Maritati na katika shule ya msingi ya Madaraka. Tumeweka mtambo wa kusukuma maji katika visima vya Kisima ambao utasukuma maji hadi kwa tangi la Madaraka, na soko la Ngusishi. Mradi wa maji wa Koome - Machaka unaotoka Ntirimiti hadi Subuiga ambapo tangi la lita elfu mia moja( 100,000) limejengwa, umekamilika. Matangi mengine ya lita elfu miambili na tano (225,000) yamejengwa huko; Ntumburi, Mucheene, Nkando, Marurui, na Mugae. Miradi mingine ni pamoja na urekebishaji wa laini ya mifereji ya kutoka Ndumira hadi Njuruta , laini mfereji ya kwenda kwa tangi la Ndumira na ujenzi wa mfereji wa kilomita sita kutoka Ndumira hadi kwa Koome. Hii ni pamoja na uunganishaji wa maji eneo la Kirune na vituo viwili vya kuuzia maji. Mradi huu utafaidi Zaidi ya watu elfu moja (1000) katika wodi ya Ruiri Rwarea. Katika wodi ya Kiirua Naari, kwa mradi wa maji wa Nturukume, tumejenga mfereji kutoka Kathita hadi eneo la Gitimene. Mradi huu utafaidi Zaidi ya wakaazi elfu tatu (3,000). Katika wodi ya Kibirichia, ujenzi wa mfereji wa mradi wa maji wa Cianteere utakaofaidi wakaazi wa Machaka, pamoja na Kivukio cha mradi wa maji wa Kiamiogo, umekamilika. Mradi huu utafaidi watu elfu tano (5000). Hivi majuzi mradi wa maji wa Mukeremi ulinufaika kwa mifereji iligharimu shillingi millioni tatu. (3,000,000) Katika gatuzi ndogo la Imenti ya Kaskazini, tangi la lita elfu mia mbili na ishirini na tano limejengwa katika eneo la Kithoka. Katika eneo la Giaki na Thuura tumeongeza laini ya mifereji na hivyo kufikia mboma Zaidi ya mia tano (500). Katika wodi ya Ntima Magharibi, tumekamilisha ujenzi wa mfereji kutoka Mto Kathita hadi vijiji vya Mpuri, Nthimbiri. Mradi huu utafaidi jamii elfu moja (1,000). Katika gatuzi ndogo la Imenti Kusini, marekebisho ya mfereji unaosambaza maji katika mji wa Nkubu na vitongoji vyake, yamekamilika. Marekebisho na upanuzi wa mradiwa maji wa Gikui-Mweru huko Igoji umekamilika huku walionuifaika nao wakiwa ni wakaazi wa soko la Igoji, na eneo la Kieni Kia Ndege. Mradi huu utafaidi Zaidi ya wakaazi elfu moja (1000) Pia tumejenga matangi katika maeneo ya Mitunguu, Kionyo na Nkuene. Katika gatuzi ndogo la Imenti ya Kati, ujenzi wa mfereji kutoka Mto Thingithu hadi soko la Kiamuri kupitia mpaka wa Meru-Tharaka umekamilika. Mradi huu una vituo kadhaa vya kutekea maji. Mradi huu utakimu Zaidi ya wenyeji elfu tatu (3000). Marekebisho ya mfereji wa Gatimbi unaonuiwa kuinuwa viwango vya maji Kwa wenyeji umekamilika. Zaidi ya hayo, matangi ya lita elfu mia mbili na ishirini na tano yamejengwa katika vituo hivi; Chaaria, Githongo, na Mwanganthia. Idara ya maji imestawisha idara ya usorovea wa maji na uchimbaji visima. Idara hii iko na vifaa mahususi vya kisasa ambavyo ni kama ifuatavyo. • Mashine/Rigi ya kuchimbua visima. • Mashine ya kutoa msukumo na kupeleleza • Mtambo maalumu wa Geodetic GPS na ulainishaji na zinginezo. Kwa sasa idara ya maji imechimbua visima kumi na vitano kikamilifu. Visima viwili huko Lubunu, viwili Thuuru na moja moja maeneo ya Barubaru, Rumanthi, Kalimbene kangeta, Maili Tatu, Githongo, Kimacia, Ntunene, Mutuati, Karichuu and Kiromwathi. Kutumia mashine yetu spesheli visima vitano vimekamilika vikiwemo; Shule ya upili ya Ntunene(wadi ya Ntunene), kijiji cha Kimachia, Shule ya msingi ya Mutuati (wadi ya Naathu) Karichu na Kiromwathi wadi ya Antubetwe Kiongo. Visima vingine ambavyo vilichimbwa bila mafanikio ya kupata maji ni shule ya msingi ya Mariri, Kijiji cha Ndulu, soko la Kithetu, na Kamboo. Kuhakikisha mazingira safi, idara ya maji na mazingira imezingatia mapendekezo ya idara ya taifa ya mazingira (NEMA) katika utunzaji wa sehemu sehemu za kutupa takataka za Murera, Nkunga na Muungu. Sehemu ya kutupa taka ya Makiri ilihamishwa mpaha Murera kwa vile ingeweza kusababisha hatari yamaradhi kwa binadamu. Vyombo vya ukusanyaji taka vimestawishwa maeneo ya Timau, Maili Tatu, Kangeta, KK,Maua, Mikinduri,Mitunguu,Kieni Kia Ndege, ,Muthara, Kianjai, Kiirua na lile na mji wa Meru. Hatua hii itaakikishia wananchi usafi katika soko zetu. Idadi ya wafanyakazi wa kudumisha usafi imeongezwa na lori tano za kubebea taka zimenunuliwa. Sehemu za misitu zimetunzwa vizuri kuhakikisha ewa safi na msururu wa mvua. Tumejenga ua la kuzingira misitu sehemu za Ngaciuma, Mporoko na Igane na juhudi zaidi zimepangiwa Rugucu, Murera, Mariara, Kithinu na Thingitho . Vilevile, tumesambaza mifereji ya maji kwa vikundi mia saba themanini (780) kwa wadi zetu. Mifereji hii inafikia zaidi ya kilomita mia sita hamsini (650 km) kwa jumla. Mradi huu ulitugharimu shillingi milioni nane (8m ) kwa kila wadi, ikiwa ni milioni tatu mwaka wa 2013/2014, milioni mbili (2), mwaka wa 2014/2015 na milioni tatu (3), 2015/2016 na kufaidi familia laki moja(100,000). Tumejenga matangi hamsini na tano (55) ya kuhifathi maji ya mvua yenye uwezo wa kuhifadhi lita laki mbili, elfu ishirini na tano (225,000 liters) kwa tangi moja katika sehemu mbali mbali zenye uhaba mkubwa. Vilevile, tumepeana matangi mia saba na kumi na tano (715) ya plastiki yenye uwezo wa kuhifadhi lita elfu kumi, na elfu tano. Matangi haya yamepeanwa katika shule za chekechea, shule za msingi, na masoko. Waheshimiwa wabunge, mahitaji ya maji mjini Meru na miji mingine ya gatuzi letu imeongezeka pakubwa kwa miaka ya hivi majuzi. Serikali yangu iko makini kupambana na swala hili na ina mipango mahususi kushughulikia swala hili kupitia kuboresha miradi ya usambazaji maji ya miji na vitongoji husika. Katika mji wa Meru, eneo la usambazaji ni kilomita mia moja arobaini mraba (140 km2) na sehemu zilizofikiwa ni kilomita sitini na nane mraba (68k km2) na unganisho za maji ni elfu tisa mia nane (9,800) zikihudumia idadi ya watu elfu arobaini na tano, mia tatu thelathini na sita (45,336). Kama mbinu ya kujaza pengo linalobaki katika mahitaji ya maji, uwezo wa kituo cha uboreshaji maji (water treatment plant) umeimarishwa kutoka lita milioni nne nukta moja tano (4.15 liters) hadi lita milioni kumi (10,000,000 liters) kwa siku. Nilizindua mradi huu wiki mbili zilizopita katika kampuni ya usambazaji maji ya MEWAS mjini Meru. Kwa hivyo maeneo ya Gikumene, Kithoka, Nkabune na Chugu yataweza kufikiwa. Usambazaji maji katika sehemu za Makutano na Kigure yameimarika pakubwa. Idara ya maji imestawisha kutuo cha udhibiti ubora wa maji (Quality analysis unit) inayochunguza ubora wa maji yanayotumiwa na wakaaji wa gatuzi letu. Lengo lake kuu ni kupunguza viwango vya maradhi yanayoambukizwa kutokana na maji. Hatua hii itapunguza mzigo wa matibabu hivyo basi rasilmali inayotumika katika maendeleo itaongezeka. Kwa sasa kuna mahabara tatu za maji zinazofanya kazi katika miji ya Maua, Meru na Nkubu. Mahabara ya mji wa Meru iko kwenye jumba la kisasa la gorofa na jingo jingine katika eneo la Kinoru kituo cha mifugo (Kinoru livestock center) linafanyiwa ukarabati ili kutumika kama mahabara ya ziada yenye uwezo wa kupima kemikali na bacteria kwenye maji. Bidhaa bora za kisasa za upimaji zimenunuliwa na maafisa watatu wa kutekeleza shughuli hii kuajiriwa. Kama njia ya kutafuta suluhu ya kuduma katika huduma za maji, tumetoa ramani za ujenzi wa mabawa matatu makubwa yatakayosaidia katika usambazaji wa maji katika kila eneo la kaunti yetu. Mabawa haya yatakuwa Kianjuri sehemu za Imenti, Thangatha sehemu za Tigania na Ura sehemu za Igembe. Mabawa haya yatagharimu mabilioni ya pesa ambayo serikali za gatuzi haziwezi kumudu na yanahitaji ufadhili kutokana na bajeti ya maji ya Serikali kuu. Mnamo tarehe kumi na mbili (jana) nilitia sahihi mkataba wa ueleano kwa niaba ya serikali ya gatuzi letu kuanzisha mradi wa unyunyizaji maji (irrigation scheme) katika maeneo ya Buuri, wenye dhamani zaidi ya milioni mia tatu na nane (308,000,000 m). Hatua hii itaboresha uzalishaji wa chakula hivyo basi kukimu mahitaji ya jamii. ELIMU Katiba ya nchi yetu imetaja elimu kama haki ya msingi ya kibinadamu. Serikali yangu imejitolea kuimarisha elimu bora katika sehemu zote za kaunti yetu. Kwa juhudi hizo, tumeajiri walimu elfu moja mia mbili na watatu (1,203) na tuko katika harakati ya kuajiri mia nne (400) zaidi mwezi huu wa Aprili ili kuboresha masomo katika shule za chekechea. Walimu hawa wameajiriwa kwa misingi ya kudumu na watapewa marupurupu pamoja na malipo ya uzeeni hali kadhalika wamewezeshwa kupata bima ya afya. Tumejenga madarasa mia moja thelathini na tano (135) katika wadi zetu zote, na tunatarajia kukamilisha na kufungua tisini (90) zaidi mwaka huu wa 2017/2018. Kadhalika, serikali yangu imeajiri walimu-wakufunzi mia moja (100) wa vyuo vya kiufundi. Vilevile tumeboresha vyuo ishirini na vitatu (23) vya kiufundi na tukapatia kila chuo vifaa na mashine za kufundishia. Jambo hili litawezesha vijana wetu kuwa na ujuzi wa kiufundi na kuweza kujitegemea. Ili kuimarisha ujuzi wa kiufundi serikali yangu imejenga karakana (workshop) ishirini na tatu (23) na kumi (10) zaidi zinapangiwa. Tayari Karakana za Maua, Thitha, Ithima, Muthara, Anthwana, Kianjai, Mituntu, Mweronduu, Kithiiri, Kithoka, Mwiteria, Karurune, Gitugu, Miugune, Kiirua, Naari,Githongo, Kiamakoro, Gitie, Nkubu, na Kanyakine zimekamilika na kuwekwa vifaa. Tumejenga vyumba vya malazi (hostels) vitatu kukidhi mahitaji ya idadi ya wanafunzi katika vyuo vya kiufundi Karurune, Gitugu na Kithiiri. Kwa muda wa wiki mbili kuanzia sasa tutapeana shilingi milioni moja kama awamu ya uanzilishi wa vyuo vya kiufundi katika sehemu zifuatazo; Murungurune (Abogeta magharibi), Ontulili (Timau) na Ruibi (Kibirichia). Vyuo hivi vya kiufundi vitafunguliwa Januari 2018. Isitoshe, serikali yangu imetoa ufadhili wa milioni ishirini na moja nukta saba (21.7m) kama ufadhili wa masomo ya kiufundi. Wanafunzi elfu mbili mia saba thelathini na tisa (2,739) wamefaidika na mpango huu huku kila mmoja akipata elfu saba, mia tisa thelathini na moja (7,931) kila mwaka. Serikali yangu imepatia zaidi ya wanafunzi elfu kumi na tano (15,000) milioni mia nne na tisini na tano(495,000,000) za ufadhili kusaidia kulipia karo zao za shule hasa shule za upili na vyuo vya anuwai kwa kipindi cha miaka mitatu. Mwaka huu, tutatoa milioni mia moja thelathini na tano zaidi (135,000,000). Kwa jumla hiyo ni zaidi ya milioni mia sita na thelathini. (630,000,000). Vilevile tumeanzisha mradi wa kusomesha watoto wawili wawili kwa kila wadi walio na changamoto za karo, waliohitimu kwa alama za juu katika mtihani wa kitaifa wa KCSE kuanzia kidato cha kwanza hadi chuo kikuu kuanzia mwaka huu. Kufikia sasa wanafunzi mia moja themanini na tatu (183) wamenufaika na kundi la kwanza la wanafunzi tisini na wawili (92) wako kwenye kidato cha pili kwa sasa, na imetugharimu milioni kumi na mbili (12,000,000m). Shule za msingi na sekondari zimenufaika na maktaba mia mbili ishirini na moja (221) kupitia kwa ofisi ya mama wa kwanza wa gatuzi la Meru. ARDHI, TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO NA MIPANGO Ardhi ni kipengee muhimu cha uzalishaji. Hivyo basi serikali yangu imetilia maanani umuhimu wa kuboresha matumishi ya ardhi kama njia ya kuwezesha wakaaji wa gatuzi letu kujitegemea kiuchumi. Tumefanya juhudi kusuluhisha mizozo ya mipaka ambayo imekuwemo kwa muda mrefu. Hii ni pamoja na mpaka wa gatuzi la Isiolo pamoja na sehemu ambayo haijafanyiwa usoroveya. Tumefaulu kupata suluhu ya kudumu. Serikali yangu iliwasilisha kesi mahakamani kutatua mpaka wa Kaunti ya Meru na Tharaka Nithi, na kesi hiyo itaamuliwa hivi karibuni. Katika sehemu za juu za Athiru gaiti A, Akithii III, Kangeta, Naathu, vyeti vya umiliki ardhi vimepeanwa. Kadhalika tumekamilisha usoroveya wa Akirang’ondu B, Kiengu, Kanjoo, Kianjai, Buuri, Kitharene, Uringu I na II, Mbeu I, Kiguchwa, Athanja na Antwamburi. Wakaaji wameanza kuvuna matunda ya juhudi hizi na maisha yao yameanza kuboreka. Ili kuwezesha kuwa na nafasi za miji zenye mazingira bora ya utenda-kazi na uekezaji, serikali yangu imekamilisha kufanya mpangilio maalumu ya mji wa Meru na vitongoji vyake vikiwemo Ntima Magharibi (Gikumene), Ntima East (Thimangiri), Municipality (wadi nzima), Nyaki West (Kithoka na Kaaga). Vilevile, tunamalizia mipangilio maalum (Integrated Strategic Urban Development Plan) kwa miji ifuatayo: Nkubu, Maua, Timau, Turingwi, Laare na vitongoji vyayo. Kupitia mipango hii tunadhihirisha kujitolea kwetu katika kuhakikisha mwelekeo unaofaa wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Baada ya kukamilisha mipangilio ya miji yetu, serikali yangu itaweza kutoa hati miliki (leases) kwa wakaaji ambayo itawasaidia katika shughuli mbalimbali za kujiendeleza kiuchumi. Nina furaha kuwajulisha kuwa gatuzi letu lilichaguliwa kuanzilisha mpangilio wa miji maalumu ujulikanao kama Symbiocity. Mradi huu unatekelezwa na shirika la Symbiocity Kenya na Baraza la Magavana na kufadhiliwa na ubalozi wa Sweden humu nchini. Tunatekeleza mradi huu kupitia mji wa Likii karibu na mpaka wa Laikipia na tumetayarisha ripoti ya kuonyesha miji hii ina uwezo wa uendelezi na ripoti hiyo itafuatwa na ufadhili wa shilingi milioni arobaini fedha zitakazotolewa kwa wote wenye mradi huu. Ajenda yetu ya kimaendeleo imewekwa katika mpangilio maalum wa County Integrated Development Plan (CIDP). Mpango huu unatuongoza kuafikia malengo yetu ya gatuzi la rangi ya kijani, kielezo, lenye umoja na ufanisi. Kupitia idara ya mipango ya kiuchumi, tumeweza kuwa na mpango wa kimaendeleo wa kila mwaka unaosimulia mambo tutakayoafikia kwa mwaka wa kifedha. Mipango hii hutusaidia katika upangaji wa bajeti na kuambatanisha na ruwaza ya Meru Rising ya 2013 pamoja na uafikiaji wa malengo ya maendeleo endelezi. Pia tunachukua na kuhifadhi takwimu ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mipango yetu ya kimaendeleo una ushahidi. Vilevile tumeimarisha uchunguzi (Monitoring and Evaluation) na kutoa sera ya kwanza ya Meru ya uchunguzi ili kutuwezesha kuboresha utendakazi. Kuhusi sera ya kuunganisha maendeleo na sayansi na teknolojia ya mawasiliano, tumeweka vifaa vya msingi vya kiteknolojia vya kuunganisha na kutoa huduma. Hali kadhalika, tumeuda kitengo cha mawasilioano ambapo wananchi wanaweza kutufikia muda wowote. Nambari ya kituo hiki ni 0709 241 000 USHIRIKA, BIASHARA NA UTALII Sekta ya vyama vya ushirika imedhihirisha ukuaji wa hali ya juu kuliko sekta zingine katika gatuzi letu. Mwanzoni mwa mwezi Decemba mwaka wa 2016, Gatuzi letu lilitajwa kama gatuzi bora zaidi katika kuimarisha vyama vya ushirika humu nchini. Tangu tuliposhika hatamu za uongozi, tumesajili vyama mia moja ishirini na tatu (123) vipya vya ushirika. Sako ishirini na saba (27) zimeanzishwa kwa madhumuni ya kupambana na umaskini na kuzalisha rasilmali. Kuna Sako za vijana, wamama na wafanyabiashara wa jumla. Kupitia uongozi na usimamizi bora wa idara ya Vyama vya ushirika, biashara na utalii, jumla ya shilingi milioni mia moja thelathini na tano (135,000,000) imepeanwa kama mtali (seed capital), na shilingi milioni mia nne themanini (480,000,000) kama akiba na mikopo hivyo basi kubadilisha maisha ya maelfu ya wakaaji wa gatuzi letu. Ili kukimu mahitaji spesheli, tutazidua Sako za walemavu na Waislamu kwa muda wa wiki moja kutoka sasa. Kathalika tumesaidia wanachama wa mashirika ya maziwa kupata vyombo mia mbili (200)vya usafirishaji maziwa (milk cans) hivyo basi kuboresha mapato yao. Mwaka huu wamepokea jumla ya shillingi milioni mia nane ishirini na tatu, mia sita ishirini na nne elfu, mia tisa na kumi na tano (823,624,915) ikilinganishwa na milioni mia tatu arobaini na nane, themanini na nne elfu, mia moja na thelathini na nane (348, 084, 138) mwaka wa elfu mbili na kumi na tatu (2013). Jumla ya mikopo iliyopeanwa na sacco zote mwaka huu ni bilioni sita, milioni mia nne sabini na sita, mia sita themanini na moja elfu, mia nne na tisini. Akiba ya jumla ya mashirika yote mwaka huu ni bilioni tano, milioni mia tatu na ishirini na mbili, mia tatu tisini na tisa elfu, mia tano arobaini na tisa (5,322,399,546). Serikali yangu imepiga hatua katika ufufuzi na uimarishaji wa sekta ya kahawa. Tumeekeza katika ufufuzi, upataji wa leseni na uimarishaji wa kiwanda cha Kisaga Kahawa cha Meru (Meru Coffee Mill). Tumewaleta pamoja zaidi ya wakulima laki moja (100,000) wa kahawa ili kusaga na kuuza mazao yao kwa hicho kiwanda. Tangu kuanzishwa, kiwada hicho kimetengeneza kahawa safi tani elfu mbili mia tano (2,500) ambayo imewaletea wakulima mapato ya shilingi bilioni moja nukta sufuri tatu (Shs 1.03b). Kutokana na mpango huu bei ya kahawa imepanda kutoka shilingi arobaini (shs 40) kwa kilo mwaka wa 2013 hadi shilingi sitini na saba na centi hamsini (67.50) mwaka wa 2016 hivyo basi kusababisha muamko na mtazamo mpya katika ulimaji wa kahawa. Kama njia ya kuhakikisha mazingira bora ya kufanyia biashara, serikali yangu imehakikisha kuwa soko ishirini na tano zimefaidika na ujensi wa ua (perimeter fence), na vivuli (market sheds). Soko la Gikumene limetandazwa na kulainishwa. Masoko ya Timau, Chaaria, Thimangiri, Antubetwe Kiongo, Mutuati, Mikinduri, Kiani kia Ndege, Kiirua, Gitimbi, Mulika, Kiorimba, Kithurine, kangeta, na Nchiru zimejengewa ua la kuzingira (perimeter fence). Soko za Kariene, Athiru gaiti, Ruiri, Kiegoi, Igoji, Laare, Kagaene, na Mikinduri zimejengewa vivuli vya kuuzia na soko za Mikinduri, Gitimbi, Kiorimba na Kithirune zimefaidika kwa ujensi wa vyoo. Soko la Kanyakine limejengewa maduka maalumu huku soko la Gakoromone likilainishwa na kuboreshwa. Ujensi wa soko zifuatazo unaendelea; Maritati, Kiria, Kunati, Kanuni, kaolo, KK, Mitunguu, Nkubu, Kiguchwa, Maua, katheri, kibirichia, Ntharene, Kagaene (kuongezewa vivuli na ua), Kiguchwa(vivuli, vyoo na ua), Athiru ruujine, Karama na Nthambiro. Kadarasi zimetolewa za ujensi wa soko zifuatazo; Ngundune, Inono, Kiutine, Miathene, Laare, karachi na Mitunguu. Soko la Miraa la Laare limekamilika. Soko tatu za mifugo zimekamilika ikiwemo Muthara, Ngundune na Kangeta. Ni muhimu kuwajulisha kwamba ujensi wa soko la Miraa la Muringene gatuzi ndogo la Igembe ya Kati ulisimamishwa kwa sababu kuna watu walienda mahakamani kusimamisha shughuli hiyo. Sekta ya Jua kali imefaidika kutokana na serikali yangu katika kila upande wa gatuzi letu kwa kupata bidhaa za zaidi ya milioni tano nukta nane. Vifaa hivi ni kama vile: Mashine tisa za kuunda ngozi, mashine tisa za ushonaji, mashine tisa za uunganishaji, mashine tisa za kuchoma vyuma na mashine tisa za usagaji. Kadhalika, idara hii ilidhamini vikundi viwili vya akina mama (Weru women group na Bettering our lives Women group) kuzuru Tanzania kuwakilisha gatuzi letu katika maonyesho ya kimataifa ya Dar es salaam ili kuonyesha bidhaa za kutoka Meru. Tumetoa mafunzo kwa wanajuakali elfu moja (1,000) ili kuwawezesha kufanikiwa zaidi katika kazi zao. Kuhusu utalii, tumeunda kijitabu kinachokusanya maneno mbalimbali kuhusu hoteli, vilabu, mahali pa kujiburundisha, na vyumba vya kulala kwenye kaunti yetu. Mwaka wa 2016 tuliandaa kongamano la tatu la ugatuzi (3rd Devolution conference katika gatuzi letu. Wajumbe zaidi ya elfu sita (6,000) walikongamana mjini Meru na kutoa fursa muhimu kuufungua mji wetu wa meru na gatuzi kwa jumla katika kufikia daraja la juu la utalii wa mikutano (conference tourism). Kongamano hili lilinuia kutathmini uafikiaji wa malengo ya ugatuzi, kukuza utalii wa ndani, utalii wa mikutano na utangamano wa wajumbe kutoka gatuzi tofauti tofauti. Nachukua fursa hii kuwashukuru waekezaji katika sekta ya hoteli wakiwemo Albar, Gatimene, Westwind, Meru Slopes Hotel, Three Stairs, Shadenet, Sierapark, Nevada na waekezaji wengine ambao wamechangia katika kuinua viwango vya huduma za mikahawa, kuuda nafasi za kazi hali kadhalika ukuaji wa jumla wa uchumi wetu katika gatuzi la Meru. IDARA YA FEDHA Idara ya fedha ina umuhimu mkuu katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kila siku katika Serikali yangu. Ili kuimarisha uwajibikaji, udhibiti wa mifumo ya kindani ya Idara imefanikishwa kwa njia mbali mbali. Kwa mfano, Serikali yangu imeunda kamati ya kuhakikisha hakuna mradi unaolipiwa bila kutekelezwa kikamilifu.Vile vile, mwongozo wa namna ya utoaji wa huduma ( service charter) umeundwa na uko tayari kutekelezwa. Hili litahakikisha kwamba masurufu (imprest) kwa wateja wa ndani yanalipwa kwa muda wa siku tatu(3) ilhali yale ya wateja wa nje na wauzaji yanalipwa kwa siku thelathini (30). Hatua hii itaridhisha wateja zaidi. Isitoshe, serikali yangu imeweka juhudi za usimamizi bora na usalama wa mali. Mali yote ya gatuzi yametambuliwa na kuwekwa nembo. Idara ya fedha ya gatuzi letu sasa inafanya kazi kwa ushirikiano na Idara ya fedha ya kitaifa ili kutekelezwa katika mitambo ya IFMIS habari zote za mali hayo. Waheshimiwa wabunge, tumechukua jukumu la kuuda na kutekeleza kisheria mashirika mbalimbali yatakayokuwa na manufaa kwa ukuaji wa uchumi wa gatuzi letu, utengenezaji wa nafazi za kazi na kuinua viwango vya uvumbuzi. Mashirika haya ni kama yafuatayo; a) Shirika ndogo la kifedha (Meru County Micro-Finance Corporation). Hili linakusudia kusaidia watu wa mapato ya chini na wasio na kazi kupata mikopo rahisi ili kuwawezesha kuanzisha biashara ndogo ndogo na waweze kujikimu kimaisha. Hadi sasa shirika hili lina matawi mawili moja katika mji wa Maua na linguine katika mji wa Meru. Kabla ya mwisho wa mwaka huu wa matumizi ya fedha za kiserikali, serikali yangu inanuia kufungua matawi mengine manne katika miji ya: Timau, Laare, Nkubu na Muriri. Hatua hii itahakikisha kwamba watu wengi zaidi wamepata mikopo zaidi na hivyo basi kupunguza makali ya umaskini. Kwa sasa zaidi ya shilingi mia moja na tatu milioni (shs 103,000,000) zimepeanwa kwa wateja elfu nne mia tano (4,500). Wateja wamejiwekea akiba ya milioni ishiri na tatu,mia tatu sabini na tano elfu,mia saba na moja (23,375,701) .mwaka wa 2015/2016 tulipokea milioni mia moja na mbili, mia mbili ishirini na sita elfu, mia tisa ishirini na tano (102,226,925) mwaka wa 2016/2017 tumepokea milioni mia moja thelathini na tatu (133,000,000) jumla ya milioni mia mbili thelathini na tano, mia mbili ishirini na sita elfu, mia tisa ishirini na tano (235,226,925) .Maono yetu ni kufanya shirika hili kuwa la kitaifa ambalo litaenea sehemu mbalimbali za Kenya na janibu zake katika Afrika mashariki, huku wamiliki wa hisa wakiwa ni wananchi wa gatuzi la Meru. b) Shirika la uwekezaji na maendeleo (Meru County Investment and Development Corporation). Takwimu za kitaifa huonyesha Meru kama mojawapo ya gatuzi zenye uwezo mkuu wa ukuaji kiuchumi hapa nchini. Waheshimiwa wabunge, mtakumbuka bayana kwamba mwaka wa 2014 mlipitisha kuundwa kwa Shirika la Uekezaji na Maendeleo katika gatuzi la Meru katika bunge hili. Jambo hili lililenga kuimarisha uekezaji kama ilivyo sera ya serikali yangu. Shirika hili linajizatiti katika kukuza rasilmali, ubunifu, kuboresha bidhaa, kukuza biashara, na kuuda nafasi za kazi kwa wakaazi wa Meru. Shirika hili la uekezaji limeanzisha mradi wa kituo cha petroli na kimekamilika katika barabara ya Mwendantu. Jambo hili litarahisisha uwajibikaji na ununuzi wa petroli kwa magari ya serikali ya Gatuzi na ya kibinafsi hivyo basi kupata pesa za kugharamia miradi mbalimbali katika gatuzi letu. Kwa sasa kuna mapatano baina ya shirika la uekezaji la Meru na National Oil Corporation (NOCK) kwa ununuzi na usafirishaji wa mafuta. Tayari kituo hiki vimetoa nafasi tano (5) za kazi na zingine zaidi zinatarajiwa wakati kituo kitaanza kutumika kikamilifu. Kwa sasa shirika hili linataraji leseni kutoka kwa tume ya kitaifa ya udhibiti wa kawi (Energy regulation commission). Hivi karibuni, waheshimiwa wabunge wa bunge la gatuzi na wananchi wote wataalikwa katika sherehe ya ufunguzi rasmi wa kituo hiki. Mkahawa wa Meru County Hotel unafanyiwa ukarabati maalum kuifanya hoteli ya kisasa. Itakuwa na dimbwi la kuogelea, vyumba vya mazoezi (gymnasium), sauna, jacuzi, vyumba vya kulala vya kifahari ili kukimu mahitaji ya kitalii na kibiashara mjini Meru. Sehemu za kupokelea wageni za kisasa zinajengwa, na ukumbi wa watu takriban mia moja. Nimetembelea na kukagua mradi huu miezi miwili iliyopita na ninaamini mradi huu utainua viwango vya utalii na huduma za hoteli hapa Meru. Tunatarajia nafasi za kazi mia moja mradi huu utakapokamilika. Kadhalika, ni muhimu kutaja kwamba kampuni ya Windlab kutoka Australia ambayo inaekeza katika kawi ya upepo Australia na Cape Town Afrika Kusini, imejitolea kuekeza katika utoaji wa megawati mia tatu katika kaunti yetu ya Meru. Awamu ya kwanza ya uchunguzi na uhusizaji jamii imekamilika na wanatarajiwa kuanza oparesheni hivi karibuni. Waekezaji wengine waliotia sahihi mkataba na serikali yangu kuzalisha kawi kutoka kwa umeme ni pamoja na Gulf Energy (kilowati mia moja) na Prunus Limited (kilowati elfu moja.) Kwa utoaji kawi safi kutoka kwa miale ya jua, kampuni ya Naanovo kutoka Uingereza imepewa kibali na Wizara ya Kawi kuzalisha megawati thelathini hapa Meru. Ufadhili wa mradi huu umepatikana na wanangoja ripoti ya mwisho ya uchunguzi kukubaliwa na serikali ya kitaifa hivyo basi kuendelea na mazungumzo ya kimauzo ya kawi baina yao na kampuni ya Umeme ya Kenya Power. Mabibi na mabwana, Gatuzi letu limejaliwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa kiwango cha kibiashara kwa kutumia mito yetu. Serikali yangu imeweza kuafikiana na kampuni ya IDEA kuunda sehemu sita ambazo zitatoa jumla ya megawati kumi na sita. Kadhalika, Absolute Energy, kampuni kutoka Italia imetenga shilingi milioni mia moja thelathini na tano (135,000,000m) kutengeneza kituo cha uzalishaji umeme chenye uwezo wa kilowati mia tatu na ishirini huko Thuura Gatuzi ndogo ya Imenti kaskazini. Vilevile mazungumzo yanaendelea ya kufadhiliwa kwa kituo kidogo cha umeme cha Gitwiki cha uwezo wa Kilowati mia sita. Waheshimiwa, changamoto inayoyakumba haya yote ni kucheleweshwa na wizara husika ya kawi kutoa kibali cha mwisho kwa waekezaji. Huku tukitambua kuwa utoaji leseni ni jukumu la serikali ya kitaifa, kucheleweshwa kwa utoaji leseni huchosha waekezaji. Hivyo basi naomba wizara husika kupitisha maombi mbalimbali yaliyo wasilishwa ili shughuli hii iweze kung’oa nanga. Sekta ya manyumba hapa Meru inaashiria ukuaji si haba. Shirika la malipo ya uzeeni (County Pension Fund) limejitolea kujenga jumba la gorofa ishirini na mbili katika mtaa wa Angaine. Ramani ya mjengo huu imekamilika na utoaji ardhi kwa shirika la uekezaji la Meru umeidhinishwa na Wizara ya ardhi ya Serikali ya Kitaifa. Serikali pia imekamilisha maafikiano nje ya mahakama na wapangaji wa hapo awali waliokuwa wameenda mahakamani kwa sababu ya mradi huu. Mabibi na mabwana, uboreshaji wa malighafi haswa ya kilimo ni nguzo muhimu katika ukuaji wa uchumi wetu.Mwaka ujao wa kifedha, Serikali yangu inaazimia kutumia shilingi milioni mia moja za kustawisha viwanda vya viazi, ndizi, asali, avocado na uundaji ngozi. Tayari mahali pa kujenga kiwanda cha viazi imepatikana Maritati eneo la Kisima. Serikali yangu pia imeafikiana na Simbanet, kampuni ya mawasiliano ili kuhakikisha mtandao wenye spidi ya hali ya juu unaunganisha gatuzi letu na ulimwengu hivyo basi kuharakisha maendeleo. Hivyo basi Simbanet itaweka vituo vya takwimu ili kuhumia serikali. Pia vijana watawezeshwa kufikia mambo mbalimbali ya kimtandao hali kadhalika masomo (e-learning) Ni muhimu kufahamu kuwa serikali yangu imenunua vifaa vya hali ya juu vya redio ya jamii ya Mugambo ywetu FM. Kama mnavyofahami, Radio hii iliporomoka baada ya bidhaa za usambazaji habari kuharibika zaidi ya miaka tatu iliyopita.Chombo hiki cha habari sasa kimefufuliwa na ni furaha yangu kuwajulisha kwamba kinapeperusha matangazo ya hafla hii moja kwa moja kupitia nambari mia moja na mbili nukta tatu (102.3FM). c) Kuundwa kwa halmashauri ya Ukusanyaji ushuru(Meru County Revenue Board). Halmashauri hii iliundwa ili kusaidia serikali ya gatuzi letu kukusanya ushuru na kutafuta mbinu nyinginezo za kuongeza mapato. Hili limesaidia serikali kuwa na wakati mzuri wa kutolea huduma. Halmashauri hii ilianza oparesheni mwaka wa 2016/2017. Ukusanyaji ushuru umeongezeka kwa asilimia kumi na sita (16 %) ikilinganishwa na mwaka wa 2015/2016. Katika hatua za kuzidisha ubora katika ukusanyaji ushuru, Bodi hii inaazimia kuafikia maofisi bora, mitambo ya utenda kazi, kustawisha utendakazi bora pamoja na risiti zilizo na vipengele visivyoweza kuigwa na kwa njia hiyo kuzuia risiti gushi (fake). Kama njia ya kuwaendeleza na kuwakuza kitaaluma, wafanyi kazi wa idara ya fedha wamepatiwa mafunzo mwafaka, ila tu shughuli hii ya utoaji mafunzo haya ni endelezi, haswa sehemu za IFMIS na kutoa ripoti za kifedha. Mwongozo wa utoaji huduma umewekwa ili kuunda msingi ambao utoaji wa huduma utakuwa nadhifu. MAPENDEKEZO YA MWAKA UJAO (2017/2018) WA KIFEDHA 1) Mafunzo ya ziada ambayo yataendelea kila wakati na ambayo yatasaidia wafanyi kazi katika idara ya fedha kuwa na viwango vya ujuzi vinavyohitajika. Ujuzi huu utasaidia utendakazi bora, nidhamu na uwazi katika mazingira ya kufanyia kazi. Zaidi ya hayo, idara ya fedha itatoa mafunzo ya kiufundi kwa idara zingine kuhusiana na uundaji wa bajeti. 2) Kwa vile mfumo wa mwongozo wa utoaji huduma umeundwa, idara ya fedha sasa itachukua hatua ya utekezaji. Inatarijiwa kuwezesha utendakazi bora na kuridhisha wateja. 3) Vilevile Idara ya fedha imegundua kwamba wateja wengi hawana uwezo wa kutumia mfumo wa IFMIS katika ununuzi haswa pale wanahitajika kutolea maelezo yao kwa mtandao. Idara hii itachukua juhudi za kuimarisha ujuzi wao. 4) Idara ya fedha inanuia kuboresha mahusiano baina yake na idara nyingine kwa kutolea mafunzo ya kifedha na utengenezaji wa bajeti. 5) Ili kuhakikisha usalama wa hati, vifaa na mali ya ofisi mbalimbali, Idara ya fedha inashughulikia mtambo wa kudhibiti wageni wanaoingia katika maofisi yetu. Hili litahakikisha kwamba ofisi za idara hii, zitaingiwa na wafanyi kazi pekee. 6) Ili kudhibitisha bei kamili, tumeunda kamati ya udhibitishaji wa miradi. Kamati hii sasa itaimarishwa ili iweze kudhibitisha bei za miradi na bidhaa, na kudhibitisha bidhaa hizo na miradi imekamilika kabla ya kulipwa. 7) Ili kukabiliana na ukosefu wa kazi na kuinua viwango vya uzalishaji wa mali, serikali yangu itajenga soko huru katika jiji la Nairobi na miji mingine (setalite markets) la wakulima litakalowezesha wazalishaji na wauzaji mazao kupata faida za juu. Waheshimiwa wajumbe, Idara ya fedha iko katika mikakati ya kuhakikisha inapata cheti kinachohitajika kutoka kwa benki kuu ili kuwezesha hili shirika la uwekezaji liweze kuchukua akiba. Hili likikamilika, hisa za shirika la uwekezaji, zitapitishwa kwa mashirika madogo ( saccos) Serikali ya Gatuzi letu imejitolea kukuza uvumbuzi kwa kuwatunuku wavumbuzi hasa katika kuinua mifumo na ukusanyaji wa ushuru. Ili kuafikia hadhi za kimataifa, Idara ya Fedha iko katika hali ya kutoa tafsiri ya utendaji kazi. Hili litahakikisha utenda kazi bora na kuafikiwa kwa viwango vya kimataifa. Ni kufuatia mafanikio haya na uvumbuzi huu ambapo Bunge letu la Seneti lilichagua Meru kama gatuzi elelezo (model County) kwa usimamizi mzuri wa rasilmali za umma na ubunifu katika kuondoa mzigo wa umaskini miongoni mwa jamii. Bunge hili linatarajiwa kuzuru Meru hivi karibuni ili kijifahamisha na jinsi miradi hii na mingine ya kimaendeleo inawezekana kwa kuzingatia asilimia ndogo ya fedha zinazofikia gatuzi hili. Baadhi ya miradi hii ni pamoja na: i. Bodi ya ukusanyaji ushuru ii. Shirika la uekezaji na maendeleo iii. Shirika ndogo la kifedha iv. Teknolojia ya probase katika ujenzi wa barabara na v. Hajira kwa walimu wa chekechea kwa misingi ya kudumu na malipo ya uzeeni. Ni furaha yangu kuwajulisha kuwa tumepokea wageni mara kwa mara kutoka gatuzi zingine wakiwa katika ziara ya kujifunza kutokana na maendeleo ambayo tumeyatekeleza. BARABARA NA UJENZI Miundomsingi bora ni muhimu katika ukuaji wa uchumi. Kama njia ya kuafikia ndoto hiyo, Serikali yangu imeimarisha barabara zaidi ya kilometa elfu moja (1,000km). Barabara mbalimbali zimeboreshwa huku barabara mpya zikifunguliwa, kutiwa changarawe (maram), vizuizi vya maji na karabati. Kwa kutumia tingatinga, barabara zimeboreshwa kilomita 35(thelathini na tano) kila wadi. Kutumia teknolojia ya Pro-base tumeuda barabara ya Kianjai-Miathene-Mikinduri (kilomita kumi) na barabara za ndani za mji wa Maua (kilomita tatu) ambayo imepata umaarufu mkubwa hapa nchini, na viongozi mbalimbali wamezuru eneo hilo kujionea njia ya bei nafuu ya kuweka lami katika barabara zetu. Ili kuunganisha sehemu mbalimbali tumejenga madaraja kwa kutumia milioni kumi na tano mwaka wa 2015/2016 na milioni arobaini na tano kwa mwaka wa 2016/2017. Soko zifuatazo zimeboreshwa kutumia teknolojia ya kabro; barabara za upande na sehemu za kuegeza magari mjini Nkubu, Steji ya Timau, Sehemu ya kuegeza magari za Makutano, eneo la Personality na steji ya Makutano steji ya Riverland, Steji ya Nkubu, eneo la kuegeza la G4S, barabara ya Makadara, na sehemu za kuegeza magari za barabara ya Gakoromone-Mikinduri, kuboresha uzoaji majimiji ya Mikinduri, Kianjai na Timau. Hatua hii imepunguza uchafu na matope mijini. Kazi ya ujensi wa teknolojia ya kabro inaendelea sehemu zifuatazo; Keeria, Mitunguu, Gatimbi, Muthara, karama, Kangeta, Kiengu, kariene, Maua, Ngushishi, laare na Mutuati. Uundaji wa barabara za ndani za mji wa Timau na Maua unaendelea. Waheshimiwa wabunge, Sehemu zifuatazo zimepangiwa kutengenezwa ka teknolojia ya kabro;sehemu za kado ya barabara za kuegeza magari za mji wa Timau, Kiutine, Mikinduri, Thimangiri, X-Lwa, Antubetwe, Maili tatu, KK, sehemu za kado ya barabara za maua za kuegeza magari,Kanyakne, Kianjai sehemu za kuegeza magari na steji. Kuboresha njia zilizoko kwenye masoko kunaendelea na kutagharimu milioni mia moja (100,000,000) 2016/2017. Waheshimiwa wabunge, ni muhimu kuwajulisha kwamba serikali yangu imelenga kukamilisha ujensi wa miji kwa kutumia teknolojia ya kabro, uwekaji wa mataa na usafirisaji maji kufukia mwaka wa 2018/2019. Kama njia ya kudhihirisha kujitolea kwa serikali yangu kuimarisha usalama, haswa masaa ya jioni, tumepiga hatua kuhakikisha kuna mwangaza wa kutosha sehemu haswa za miji za gatuzi letu. Mradi huu umebadikwa jina ‘mulika mwizi’.Mradi wa kuweka mataa kwenye miji na barabara umewezesha wananchi kuendelea na biashara zao hata masaa ya jioni kwa sababu visa vya kiuhalifu vimepungua. Zaidi ya taa themanini na mbili (82) zimewekwa kwenye miji mbalimbali na barabara za miji kama vile Meru, Nkubu, Maua na vitongoji vyayo sasa zimepata mwangaza ambao umewafaa kwa njia kuu wakaaji wa eneo hizo. KILIMO Waheshimiwa wabunge, ninafahamu kuwa ili kutuwezesha kuafikia malengo ya maendeleo endelezi ni lazima tuweke sekta ya kilimo kifua mbele kwa sababu ni uti wa mgongo wa uchumi wetu.Wakulima wamepokea mbegu yenye uwezo wa kuhimili kiangazi tani tisini na saba (97 tonnes) kama vile mtama, ndengu, mchele na mahindi sehemu zinazokumbwa na ukame. Ili kukimu mahitaji ya mbolea ya wakulima, Serikali yangu imehakikisha wakulima wamepata mbolea ya bei iliyopunguzwa. Kwa sasa tumesafirisha mifuko elfu kumi na mbili mia nne na kumi na mbili (12,412) ya kilo hamsini ambayo imefaidi wakulima elfu hamsini (50,000). Ili kuboresha uzalishaji wa maziwa, njia ya mipira imetumiwa kwa mbegu ya uzalishaji kutoka Brazil (AI) ambapo ng’ombe elfu saba mia tisa sitini na tisa (7,969) wamehudumiwa na dama elfu tano mia mbili na kumi na tano (5,215) wamezaliwa. Maafisa kumi na wanane wameajiriwa kuhudumia ng’ombe kwa njia ya mipira. Ili kuboresha ukulima wa ng’ombe wa nyama, tulizindua mradi wa fahali (Sahiwal bull), kwa vile ni vigumu kuhudumia ng’ombe wa kienyeji kwa njia ya mipira. Fahali hawa walitugharimu shilingi elfu mia moja na ishirini (120,000 shs) kila mmoja na jumla ya milioni mbili nukta nne (2.4m) kinyume na propaganda inayoenezwa na wapinzani wa Serikali yetu. Fahali hawa wamefanya kazi nzuri. Ng’ombe elfu mbili mia moja na wanane (2,108) wamehudumiwa na dama mia tatu tisini na wawili (392) wamezaliwa. Kwa sasa fahali hawa wamekuwa wazito zaidi hivi kwamba hawawezi kuhudumia ng’ombe. Tunapanga kuwapeana kwa vikundi vinavyowatunza ili wachinjwe na kufanya karamu. Baadaye tutanunua fahali wengine ili kazi hii nzuri iendelee. Tumenunua mbuzi wa maziwa elfu mbili mia nane na wanane (2,808) na wakapeanwa kwa vikundi vya wakulima. Wana wa mbuzi mia sita thelathini na watano (635) wamezaliwa Kiwada cha maziwa ya mbuzi pia kimestawishwa katika kituo cha mafunzo ya kilimo cha Kaguru. Vilevile vikundi vya wakulima vimepewa kuku wa kienyeji elfu themanini na tatu, mia sita na sitini (83,660). Kama njia ya kuzuia hasara kwa wakulima wetu , serikali imechanja mifugo ikiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo elfu mia mbili sabini na nne (274,000), kuku elfu mia mbili na kumi (210,000) hivyo basi kuzuia magonjwa kama vile kimeta (anthrax), vidoda vya midomo na miguu, kichaa cha mbwa na paka na mengineo. Kilimo cha samaki pia kimeboreshwa kwa kustawisha sehemu mbili za uzalishaji samaki. Kiwada cha samaki cha Kanyakine sasa kinaendeshwa na shirika la wakulima wa samaki wa Meru. Nwahimiza wameru wajizoeze kula samaki kama njia moja ya kuongeza proteni mwilini. Tayari dimbwi sita za kimaonyesho ya ufugaji wa samaki aina ya trout zimestawishwa. Samaki wadogo elfu kumi na mia mbili (10,200) tayari wameletwa. Pia sehemu mbili za kuzalisha samaki zimestawishwa. Dimbwi mia moja hamsini na sita zimestawishwa na tani ishirini na nane (28) za lishe ya samaki kupeanwa kwa wakulima. Wakulima wa ndizi wamesaidiwa na bidhaa za kuwawezesha kutengeneza pombe ya ndizi, na wanatarajiwa kufikia kiwango cha kibiashara. MICHEZO, VIJANA, JINSIA NA MASWALA YA JAMII Serikali yangu imejitolea kuimarisha michezo na kupalilia vipawa miongoni mwa vijana wetu. Ujensi wa uwanja wa michezo wa Kinoru unaendelea na unatarajiwa kuwa wa tatu bora zaidi humu nchini baada ya kukamilika. Mradi huu utaziduliwa rasmi Juni mwaka huu na utakuwa na uwezo wa kubeba watu elfu ishirini (20,000). Nyanja zingine zinazojengwa ni Nguthiru, Timau, Githongo, Maili- tatu, na Kirwiro Baseball Complex. Nyinginezo zitakazojengwa ni Laare, Urru,Maua na Nkubu. Uwanja mmoja kila wadi umelainishwa. King’ang’anyiro cha kombe la Gavana kinaendelea na jumla ya timu mia moja themanini (180) zinashiriki, timu nne kutoka kila wadi. Idara ya michezo imesambaza vifaa kama mipira, jeshi za wachezaji, malipo ya refa na uchukuzi wa wachezaji. Zawadi zitatolewa kila gatuzi ndogo kama ifuatavyo: Timu ya kwanza- shillingi elfu mia tano (500,000) Timu ya pili- shillingi elfu mia tatu (300,000) Timu ya tatu- shillingi elfu mia mbili (200,000) Timu ya nne- shillingi elfu mia moja (100,000) Katika kiwango cha gatuzi, timu zitatunukiwa kama ifuatavyo: Timu ya kwanza-shillingi elfu mia sita (600,000) Timu ya pili- shilling elfu mia nne (400,000) Timu ya tatu- Shillingi elfu mia tatu (300,000) Timu ya nne - Shillingi elfu mia mbili ( 200,000) Ni muhimu kutambua ya kwamba Meru imetambuliwa na shirika la kitaifa la sika FKF kama gatuzi linaloongoza katika uwekezaji fedha katika mchezo wa kandanda. Kama hatua ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya na pombe haramu, serikali yangu ilianzisha Bodi ya Kudhibiti matumishi ya pombe (Meru County Alcoholic drinks Control Board). Bodi hii imepiga hatua katia utoaji leseni, utoaji mafunzo kwa umma pamoja na wamiliki wa mabaa. Bodi hii pia ilizindua Shindano la kibiashara la (Youth business challenge) tarehe 22/10/2016. Shindano hili lilinuia kutambua na kukuza vikundi vya vijana na kina mama wenye ujuzi na mawazo ambayo yanaweza kuleta ajira na uzalishajiwa rasilmali hivyo kukuza uchumi wetu. Jambo hili pia litachangia vijana kutohusika katika matumizi ya madawa ya kulevya. Mabibi na mabwana, katika bajeti ya mwaka ujao, tutajenga kituo cha urekebishaji ili kuboresha afya na maadili haswa kwa walioadhiriwa na madawa na unywaji pombe kupindukia. Isitoshe tumepeana bidhaa za michezo kwa zaidi ya vilabu mia nne, jacketi za waendeshaji pikipiki kwa zaidi ya watu elfu nne mia tano, mipira mia tisa, mavasi ya wanasoka kwa vilabu mia tatu themanini, mavazi ya wachezaji wa voliboli tisini na neti tisini za voliboli. UTUMISHI WA UMMA Idara ya Utumishi wa Umma imekuwa ikitekeleza majukumu muhimu katika Serikali yakiwemo yafuatayo: • Kama kiungo-kati muhimu katika utoaji huduma za kijamii pamoja na usimamizi wake. • Kuajiri wafanya-kazi wa Serikali, kuwadumisha na kuwapandisha vyeo . • Kushirikisha umma katika uudaji sera. • Utekelezaji na • Kukabiliana na majanga ya moto. Tumetekeleza na kuajiri wafanya kazi kwa mtindo wa ugatuzi kutoka makao makuu hadi kwa wadi kulingana na sheria ya serikali za ugatuzi iliyopitishwa mwaka wa 2012. Vilevile tumepitisha na kutekeleza nembo (emblem) za gatuzi letu kuambatana na sheria iliyopitishwa mwaka wa 2014. Isitoshe tumenunua magari saba ya kusafirisha maafisa wa nyanjani. Tumeajiri maafisa hamsini na sita wa utekelezaji sheria za gatuzi. Maafisa hawa wamewekwa katika vituo viwili; Makutano na gakoromone. Katika kikosi hiki cha utekelezaji, tumeuda idara ya trafik ili kumudu barabara zetu na kuhudumia magari na wasafiri kikamilifu. Kama mbinu ya kurahisisha utoaji huduma, tumeajiri wafanyakazi elfu mbili mia nne hamsini na wanane. Ni muhimu kutaja kuwa tuliweza kulipa malimbikizi ya wafanyi kazi walio kuwa wa serikali za wilaya kabla ya mfumo wa ugatuzi kuanzishwa. Malipo hayo yalitugharimu shilingi milioni hamsini na tano. Wafanyi kazi mia saba sabini na sita waliingizwa kwenye mpango wa malipo ya uzeeni wa serikali ya gatuzi ama ule wa zamani wa serikali za mtaa. Tumefaulu kutenganisha viwango viwili vya serikali; Bunge la gatuzi letu na utumishi wa umma wa serikali yetu. Ili kuendelea kuboresha utenda kazi na motisha kwa wafanyakazi, tumeweka mikakati ya wafanyakazi kujikuza kitaaluma.Wafanyakazi mia tano thelathini na wanane (538) wamepandishwa vyeo na wengine mia nane hamsini na nane (858) wamehojiwa kwa madhumuni ya kuwapandisha vyeo hivi karibuni. Tunapeana bima ya afya kwa wafanya kazi inayokimu mahitaji ya kutibiwa na kurundi nyumbani, kulazwa, kujifungua, matibabu ya meno na macho. Tumestawisha idara ya elimu ya umma inayowasaidia wananchi kufahamu haki na majukumu yao ya kikatiba kuambatana na sheria ya ugatuzi iliyopitishwa mwaka wa 2012. Tumeweza kuwafikia takriban wananchi elfu ishirini na mbili (22,000). Tumepitisha na kutekeleza mwongozo wa kushirikisha umma mwaka wa 2014 (Meru County Public participation Act, 2014). IDARA YA SHERIA Kupitia ushirikano mwafaka ulioko wa utenda kazi baina ya matawi yetu mawili ya serikali, yaani serikali tekelezi na bunge la gatuzi, tumeafikikia mengi na haswa kupitisha sheria ishirini na sita katika miaka ile tumekuwa uongozini.Miaka iliyopita, Serikali yangu imedhamini na kushirikiana na bunge la gatuzi kupitisha sheria zifuatazo; 1. Sheria ya udhibiti wa vileo ( Meru County Alcoholic Drinks Control Act, 2014;) 2. Sheria ya ushirikishi umma(Meru County Public Participation Act, 2014;) 3. Sheria ya uhdibiti huduma za maji na usafi wa mazingira (The Meru County Water and Sanitation Services Act, 2014;) 4. Sheria ya utalii na wanyama-pori (The Meru County Wildlife and Conservancies Management Act, 2014;) 5. Sheria ya Almashauri ya uekezaji na maendeleo (The Meru County Investment and Development Corporation Act, 2014;) 6. Sheria ya Shirika ndogo la kifedha (The Meru County Microfinance Corporation, 2014;) 7. Sheria ya vyama vya ushirika (The Meru County Cooperatives Societies Act, 2014;) 8. Sheria ya Almashauri ya ukusanyaji ushuru (The Meru County Revenue Board Act, 2014;) 9. Sheria ya ugavi wa rasilmali (The Meru County Appropriation Act, 2014;) 10. Sheria ya ugavi wa rasilmali (The Meru County Appropriation Act, 2015;) 11. Sheria ya ugavi wa rasilmali ya gatuzi (The Meru County Appropriation Act, 2016;) 12. Sheria ya udhibiti wa kifedha wa mikopo ya magari (County Assembly of Meru Staff Car Loan Fund Regulations, 2015;) 13. Sheria ya udhibiti wa kifedha wa mikopo ya (County Assembly of Meru Staff Housing Fund Regulations, 2015;) 14.Sheria ya Udhibiti wa kifedha wa mikopo ya magari kwa wanakamati wa serikali ya Gatuzi la Meru. (Meru County Executive Staff Car Loan Fund Regulations, 2015;) 15. Sheria ya Udhibiti wa kiwango cha fedha za ujenzi kwa wanakamati wa Serikali ya Gatuzi la Meru. (Meru County Executive Staff Housing Fund Regulations, 2015;) 16. Sheria ya Uratibu wa shughuli za serikali ya Gatuzi la Meru. (Meru County Co-ordination of Government Functions Act, 2015; 17. Sheria za Utawala katika Gatuzi la Meru (The Meru County Grants (Administration) Regulations 2014;) 18.Sheria Ya Ishara Na Nembo katika serikali ya Gatuzi la Meru. (The Meru County Symbols and Emblems Act, 2016;) 19. Sheria ya Fedha Ya Serikali ya Gatuzi la Meru. (The Meru County Finance Act, 2016;) 20. Sheria ya Huduma Za Afya. (The Meru County Health Services Act, 2016;) 21. Sheria ya udhibiti wa majanga (The Meru County Disaster management act, 2016;) 22. Sheria ya udhibiti uteuzi (The Meru County Public Appointments (County Assembly Approval) Act, 2016;) 23. Sheria ya walemavu (The Meru County Persons with Disabilities Act, 2016;) 24. Sheria ya huduma za bunge la gatuzi (The Meru County Assembly Service Act, 2016; 25. Sheria ya udumishaji wa sheria (The Meru County Retention and Enhancement Act, 2016 and) 26. Sheria ya mipango ya serikali (The Meru County Spatial Planning Act, 2016.) Jambo hili linafanya gatuzi letu kuwa gatuzi lenye sheria bora zaidi hapa nchini. Tukiwa na sheria hizi, tuna msingi wa kutekeleza majukumu ya ugatuzi kwa mujibu wa katiba. Kwa hili nawashuru sana waheshimiwa wabunge wa gatuzi letu la Meru. ZIARA ZA KIMASOMO KWENYE GATUZI LETU Kama ilivyo katika mwito wetu mkuu kuwa gatuzi kielelezo hapa nchini na sehemu mbali mbali za dunia, hatua zetu za kimaendeleo zimevutia vikundi kutoka nchi na gatuzi mbali mbali. Waheshimiwa wajumbe, nina furaha kuu kuwajulisha kwamba, Idara ya Uchukuzi, Barabara na Ujensi, imetembelewa na Idara ya barabara ya nchi ya Uganda, Wizara ya kitaifa ya barabara nchini Tanzania, Wizara ya kitaifa ya bar

 

 

 

 

 

Twitter Feeds
College of Biological and Physical Sciences School of Biological Sciences
cbps.uonbisbs.uonbisps.uonbimeteorology.uonbiphysics.uonbichemistry.uonbigeology.uonbiicca.uonbicebib.uonbisci.uonbimathematics.uonbi